Baadhi ya wakulima wanaofanya kilimo kwenye maeneo kame au maeneo yaliyo nusu kame, uwekaji boji ni jambo la maana wanalofaa kutilia maanani ili mazao yawe ya kupendeza licha ya upepo mkali. Maeneo haya kwa mara nyingi huwa na upepo mkali ambao hupeperusha unyevu baada ya mkulima kunyunyuzia mimea yake maji.

Boji ya nyasi iliyokauka

Boji hutokana na matawi yaliyokauka ambayo huwekwa kwenye mizizi ya mimea ili kuzuia upepo mkali kutokausha unyevu kwani maeneo kame huwa na uhaba wa maji.Ili uwekezaji wa mkulima kwenye maeneo kame uwe wakufana, ni sharti kwanza akague hali ya upepo ,misimu ya mvua na mahali ambapo anaeza pata maji ya kunyunyuzia mimea yake.ukaguzi wa vifaa vya boji ni lazima utiliwe maanani na aina ya mimea mkulima angependa kukuza kwenye shamba lake.

Visima kwa mara nyingi hutumika kama njia mbadala ya kupata maji katika maeneo haya na ili kuzuia uharibifu wa maji boji husaidia kuzuia miale ya jua kali kwenye mizizi ya mimea na kuzuia uvukuzi wa unyevu .

mkulima anafunzwa kutumia boji

Boji mara nyingi hutumuika kama njia bora ya kuzuia ukuzi wa magugu katika shamba na kupunguza kushindania madini baina ya mimea na magugu.Njia nyingine za kuzuia magugu huharibu madini yalioko kwenye mchanga na kufanya ardhi kutokua na uzalishajui bora .Ili boji iwe na manufaa ni lazima iwekwe ikizingira mmea na unyunyuziaji ufanywe asubuhi na mapema na jioni wakati miale ya jua sio kali.

Boji ya matawi

Isitoshe kwa maeneo ambayo huwa na mvua nyingi, boji ya mawe hutumika ili joto ambalo mawe itapata iweze kutumika kuupa mmea joto wakati wa baridi kali.

Patricia M Kombo

patriciah@africafarmers.org

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *